Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bankkubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema mwezi March.
Pamoja na kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine yapatayo 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia Air Line.
Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa rafiki mmoja wa karibu na Wolper (jina lipo), anamshangaa sana shoga yake huyo kwani amekuwa akibadili namba za simu kwa mwaka mmoja hata mara saba.
“Unajua kwa maisha ya sasa, simu ikipotea mtu unairinyuu laini yako ileile, maana ndiyo inayojulikana na wadau. Lakini yule mwenzetu siyo. Nimeshamsevu kwenye simu yangu kwa majina ya Wolper, Wolper Tena, Wolper Nyingine, Wolper Nyingine Kabisa na Wolper Hakuna Tena, lakini zote kwa sasa hazipo hewani,” alisema shoga yake huyo huku akicheka.Wolper alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi iliyozoeleka, hakupatikana. Jitihadi zilifanyika akaja kupatikana kwenye namba mpya ambapo alisema:
“Mimi nikishapoteza laini naona uvivu kwenda kuirinyuu, ndiyo maana nanunua nyingine.”